Mwanamuziki nyota, Shakira amefunguliwa mashtaka na mwanamuziki kutoka Cuba, Livana akimtuhumu kuchukua kipande kidogo cha wimbo wake alioandika miaka kumi iliopita bila ruhusa yake.

Wimbo huo ulipata umaarufu mkubwa ‘Bicicleta’ ulioimbwa na Shakira pamoja na Vives ulishinda tuzo za Gramyy miongoni mwa mataifa ya Latino mwaka uliopita.

Livan anadai kuwa Shakira na Vivez walinakili mistari na kipande kidogo cha kibwagizo cha wimbo wake wa 1997 Yo Te Quiero Tanto {I Love You So much} iliyotolewa na kampuni ya muziki ya Sony.

Mahakama ya Uhispania ambapo Shakira anaishi itachunguza madai hayo kama yamnamuhusu mwanamuziki hyuo.

Kutokana na madai hayo upande wa Shakira umekataa kuzungumza kuhusu kesi hiyo  iliyofunguliwa na mwanamuziki huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *