Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.
Kisa hicho kilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo siku ya Jumanne muda mfupi baada ya wageni hao kuwafunga Celtic bao la tano.
PSG pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo.
Kesi hiyo itaangaziwa na kitengo cha maadili na nidhamu katika shirikisho la Uefa tarehe19 Octoba.
Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.
Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri.
Inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya.