Staa wa Bongo fleva, Sara Kaisi maarufu kama Shaa amesema wimbo wake mpya “Sawa” utakuwa na video mbili tofauti.

Shaa amesema kwamba video ya kwanza imefanywa chini ya muongozaji kutoka nje ya nchi, Justin Campos ikiwa maalumu kwa ajili ya kuonesha swaga zake pamoja na fashion kwa ujumla.

Staa huyo amesema video ya pili ya wimbo wake huo imefanywa na muongozaji Nick Dizzo kutoka hapa hapa nchini ambapo video hiyo imebesi sana kwenye kucheza tofauti na ile aliyoifanywa kwa Justin Campos.

Shaa ni miongoni mwa wanamuziki wa kike wanaofanya vizuri nchini kwasasa ambapo tayari staa huyo ameanzisha lebo yake mwenyewe kwa ajili ya kusimamia kazi zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *