Serikali imezuia mali zote za watuhumiwa wa kesi ya Escrow Singh na mwenzake Rugemarila ambapo Mali zote zimewekwa chini ya ulinzi mkali na account zao pia benki zimefungwa.

Pia imeelezwa orodha ya waliokwapua pesa za Escrow na kugawana imeongezeka wapo vigogo kutoka wizara ya fedha, taasis za dini, maaskofu, NGOs, na wataanza kuhojiwa kuanzia jumatatu ili nao wafikishwe mahakamani.

Imeelezwa kila aliyehusika atafikishwa mahakama bila kubagua wala kujali nafasi yake katika jamii.

Taarifa zaidi zinaeleza wanaotuhumiwa katika sakata hilo wanakaribia 30.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani kutokana na kesi hiyo Escrow inayowakabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *