Serikali imesema itaanza zoezi la kuajiri watumishi wapya punde tu itakapokalimisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa nchini.

Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Angela Kairuki amesema kuwa jumla ya ajira elfu 71 zinatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha.

Waziri huyo amesema ukiangalia katika mwaka huu wa fedha ajira ambazo wanatarajia kuzitoa katika serikali ni takribani elfu 71.

Pia waziri huyo amesema anapenda kuwatia moyo kuwa wasomi waendelee kusubiri wasijiinge katika makundi ambayo hawastahili kuingizwa waendelee kuwa na uadilifu na muda si mrefu wataingia katika utumishi wa umma.

Kwa upande mwingine Waziri Kairuki amesema serikali imebaini watumishi hewa 16,127 baada ya kufanya zoezi la kuhakiki katika idara na taasisi zake zote nchini kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *