Serikali imesema ipo tayari kugharamia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo familia itaomba jambo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy  amesema kwamba kama familia itahitaji na ripoti ya madaktari ikionyesha kuna ulazima wa Tundu Lissu kupatiwa matibabu zaidi, serikali itasimamia suala hilo.

Hivi karibuni kumekuwa kukiendeshwa kampeni ya kuchangia matibabu ya Tundu Lissu baada ya gharama zake za matibabu kuwa kubwa huku baadhi ya watu wakiitupia lawama serikali kwa kushindwa kusimamia hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *