Waziri wa fedha na bajeti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pierre Kangudia amesema kuwa nchi hiyo haitaweza kutafuta fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa rais mwaka huu.

Makubaliano baina ya pande mbili, upande wa upinzani na serikali iliyoko madarakani kwa pamoja walikubaliana kuwa uchaguzi huo ungefanyika mwishoni mwa mwaka huu wa 2017.

Waziri huyo amesema kwamba kwa muujibu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba uchaguzi huo gharama yake ni dola bilioni moja nukta nane zikiwa ni fedha za maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe.

Wapinzani wa rais Joseph Kabila wamekuwa wakimtuhumu kwa kurejelea kuchelewesha uchaguzi kwa lengo la kusalia madarakani.

Rais Joseph Kabila alikwisha maliza muhula wake kama rais wa nchi hiyo December mwaka wa jana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *