Serikali imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa kituo kipya kikubwa cha kuzalisha umeme unaoanzia mkoani Iringa hadi Shinyanga.

Asilimia 99% ya ujenzi huo umekamilika na kiinategemewa kuanza uzalishaji wa umeme Oktoba mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO, Mhandisi Felichesmi Mramba amesema kuwa kituo hicho kipya cha kuzalisha umeme kinalenga kupunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika maeneo ambayo yatapitiwa na mradi huo.

 

Mhandisi Mramba amefafanua kwamba hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli ya kutaka shirika hilo liboreshe uzalishaji wa umeme ili kuliwezesha taifa kuwa nchi ya viwanda.

 

Pia ameongeza kwa kusema kwamba serikali inajenga njia ya umeme ya kuunganisha mikoa ya Mtwara na Lindi itakayozalisha Kilovoti 132 na kama kazi hiyo wangepewa makandarasi wa nje ingegharimu pesa nyingi lakini kazi hiyo inafanywa na wakandarasi wa ndani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la kuwatumia wahandisi wa ndani katika ujenzi wa miundombinu ndani ya nchi.

 

Vile vile Mhandisi Mramba amesema katika kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma wanatarajia kutumia Shilingi Bilioni 60 kwaajili ya kuhimarisha miundombinu iliyopo na kujenga miundombinu mipya ya kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Dododma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *