Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali itajenga vyumba vya upasuaji 170 kwa wajawazito ili kupunguza vifo vya mama wajawazito.

Waziri Ummy amesema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 80  kufika 2025.

Pia waziri Ummy amesema kuwa msaada wa mashine hiyo ya kutoa dawa ya usingizi kutoka Utepe Mweupe utaisaidia kupambana  kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa asilimia 40 kufikia 2020 nchini.

Aidha Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya afya kuongeza wataalamu wa kutoa dawa ya usingizi wakati Serikali ipo katika mkakati wa kuongeza vifaa na dawa kwenye vituo vinavyotolea huduma ya afya hasa uzazi.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imejiongeza kwa kutenga bilioni 8 kwa ajili kununua dawa za uzazi salama  ikiwemo dawa za kuzuia kifafa cha mimba,kuzuia mama kuvuja damu na hupatikana bila ya gharama yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *