Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea kuliboresha shirika lake la ndege nchini ATCL ikiwa ni pamoja na kuchukua madeni yake mbalimbali ili kuhakikisha shirika hilo linafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Dkt Mpango ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya Wizara hiyo ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

Waziri huyo amesema kuwa “Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali amekamilisha ukaguzi wa shirika letu la ndege, ilikukamilimisha mizania ya kampuni, lakini tumeamua kuyachukua madeni yote ya ATCL ili kuweza kusafisha hiyo mizania,”.

Pia amesema kuwa“Muheshimiwa Rais ameteua bodi mpya ya wakurugenzi ambayo inaweledi katika mambo ya usafirishaji wa anga, menejimenti mpya lakini kuhakikisha shirika linakuwa na mpango wa biashara wa muda wa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka mwezi Juni mwaka huu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *