Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inatarajia kuanzisha mkoa wa kipolisi wilayani Rufiji.

Nchemba amesema hayo leo Bunge katika hutoba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017 /18.

Kusogeza huduma ya kipolisi karibu zaidi na wananchi na kurejesha amani na utulivu katika maeneo hayo na wilaya ya Mafia nayo itakuwa ndani ya mkoa huo mpya.

Nchemba amesema Mkoa huo utaitwa Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji ambao utajumuisha wilaya za Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo.

Waziri Nchemba amesema kuwa mkoa huo wa kipolisi utasaidi kupungua kwa matukio mbalimbali ya mauaji ambayo yamegharimu maisha ya baadhi ya wananchi wilayani humo.

Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga yamekithiri kwa mauaji ya raia pamoja na askari polisi ambapo baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mauaji hayo.

Baadhi ya matukio ya hivi karibuni ni kuuawa kwa askari Polisi wanane wakati wakirudi kwenye doria wilayani Kibiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *