Kipa namba mbili wa klabu ya Manchester United Sergio Romero amesaini mkataba mpya wa miaka minne utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2021.

Romero, mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na mashetani wekundu wa Old Traford mwaka 2015 akitokea timu ya Sampdoria.

Kipa huyu namba moja wa timu ya taifa ya Argentina amecheza michezo 28 katika misimu miwili aliyoichezea timu yake na katika michezo hiyo ni michezo sita tu aliyocheza katika ligi kuu ya England.

Tetesi za golikipa namba moja wa Man United, David De Ge kuwa anaweza kusajiliwa na Real Madrid, huenda zikawa zimechangia kwa kipa huyu kuongeza mkataba mpya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *