Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero ameadhibiwa na chama cha soka nchini Uingereza baada ya kumpiga kiwiko beki wa West Ham United, Winston Reid kwenye mechi ya ligi kuu iliyofanyika jumpili.

Aguero amefungiwa jumla ya mechi tatu ambapo mbili zikiwa za ligi kuu dhidi ya Manchester United Sepetemba 10 na Bournemouth Septemba 17

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia ataukosa mchezo wa kombe la ligi EFL dhidi ya Swansea.

Sergio Aguero: Akimpiga kiwiko beki wa West Ham United Winston Reid kwenye mechi ya ligi kuu jumapili iliyopita ambapo City ilishinda 3-1.
Sergio Aguero: Akimpiga kiwiko beki wa West Ham United Winston Reid kwenye mechi ya ligi kuu jumapili iliyopita ambapo City ilishinda 3-1.

Referee Andre Marriner alishindwa kumuona mshambuliaji huyo wakati akifanya tukio hilo na kushindwa kumtoa nje kwenye mchezo huo ambapo City walishinda 3-1.

Pia mshambuliaji huyo ameachwa kwenye kikosi cha Argentina kwa ajili ya kucheza mechi ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 kutokana na kuwa majeruhi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *