Timu ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeondoka leo kuelekea Rwanda kwa ajili ya kambi ya siku 10.

Serengeti inajiandaa na mechi ya marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wa umri huo dhidi ya Congo Brazzaville inayotarajiwa kuchezwa wiki ijayo.

Katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita, Serengeti iliiadhibu Congo kwa mabao 3-2 kupitia kwa Yohana Mkomola aliyefunga magoli mawili kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa na Issa Makamba kipindi cha pili.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kuwa wachezaji wana ari na kwamba mlinda mlango Kabwili anaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa timu hiyo aliokosa mechi ya kwanza wamerejea kikosini na watacheza mechi ya marudiano.

Katika mchezo wa marudiano dhidi ya Congo utakaofanyika Oktoba 3 Serengeti inatakiwa kucheza kufa au kupona isiruhusu kufungwa ama ishinde ili ikate tiketi ya kucheza fainali hizo mwakani Madagascar.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *