Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jana imetoka 0-0 na Mali katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika.

Mali walioutawala sana mchezo huo kutokana na Serengeti Boys kucheza kwa tahadhari ya kujihami zaidi kuliko kushambulia.

Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu na kupanga vyema mashambulizi yao, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania ilicheza vizuri na kuokoa hatari nyingi.

Kipa wa Tanzania, Ramadhani Kabwili alifanya kazi ya ziada baada ya kuokoa michomo ya hatari kutoka kwa washambuliaji wa Mali.

Kwa kutumia mfumo wa kushambulia kwa kushitukiza, Serengeti Boys nayo ililikaribia mara kadhaa lango la Mali, lakini wakashindwa kutumia nafasi.

Serengeti Boys ilipata nafasi za kufunga kipindi cha pili, huku nafasi nzuri zaidi akiipoteza Assad Ally ambaye akiwa amebaki na kipa wa Mali na kukosa goli la wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *