Serengeti Boys imeshinda 1-0 dhidi ya Northern Dynamo kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika katika mji wa Viktoria katika visiwa vya Shelisheli.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili kutokana na kushambuliaana mara kwa mara.

Serengeti Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi watano, wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo imerejea nchini kwa ajili ya mchezo wake Septemba 18 nwaka huu.

Mchezo huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Fainali hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili 2017.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *