Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ imefuzu kushiriki fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Gabon, Aprili mwaka huu baada ya rufaa yao kukubaliwa.

Serengeti imefuzu baada ya kushinda rufaa waliiyomkatia mchezaji wa Congo Brazzaville, Langa-Lesse Bercy anayedaiwa kuwa na umri mkubwa aliyetakiwa kwenda kupimwa vipimo maalum cha kuthibitisha umri halisi.

Taarifa zilizopatikana jana Ijumaa jioni kutoka mkutano wa CAF nchini Gabon zilidai Serengeti ilipewa nafasi hiyo na sasa itakuwa kati ya timu 8 zitakazocheza fainali hizo.

Waziri wa Michezo, Nape Nnauye ameipongeza timu hiyo katika ujumbe wake kupitia akaunti yake ya Twitter.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *