Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imetolewa katika michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa 1-0 na Niger.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho wa Kundi B ulifanyika katika Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil nchini Gabon.

Niger na Tanzania zina alama sawa na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao amefuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo Niger inaungana na Mali ambayo inaongoza kundi kwa pointi zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zikiaga mashindano hayo.

Serengeti Boys ilizidiwa katika mchezo huo kwa kipindi cha kwanza na cha pili hali iliendelea kuwa hivyo na hatimaye Niger wakatoka kifua mbele kwa kuitoa Tanzania.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *