Timu ya taifa ya umri chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys huenda ikashiriki katika fainali za Afcon 2017 zitakazofanyika Madagascar baada ya mchezaji waliomkatia rufaa kukataa kufanyiwa vipimo.

Mchezaji huyo wa Congo Brazaville, Langa Lesse Bercy alitakatiwa rufaa na Tanzania kutokana na madai ya kuzidi umri, ameshindwa kutokea kwenye vipimo vya mifupa vilivyokuwa vifanyike jijini Cairo Misri juzi.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipeleka Ujumbe wa watu wanne kwa ajili ya zoezi hilo, ambalo lilikuwa lifanyike juzi lakini halikufanyika baada ya mchezaji huyo kutofika kwa kile kilichoelezwa eneo analoishi kuwa na vita.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa mchezaji huyo hakutokea kwenye vipimo kutokana na sababu hizo ambazo hawana uhakika kama ni za kweli kwakuwa hawajapata taarifa zozote za kutokea vita nchini Congo.

TFF wamelipia gharama zote za vipimo na za watu wote watakaohusika lakini mpaka sasa haijafahamika kama watarudishiwa pesa zao kutokana na zoezi hilo kutofanyika.

Mwaka 2004 Tanzania ilipokonywa nafasi ya kushiriki fainali za vijana wenye umri chinia ya miaka 17 za mwaka 2005 baada ya mchezaji wake Nurdin Bakara kuzidi umri.

Caf huenda ikaipa nafasi Serengeti Boys kucheza fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *