Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 “Serengeti Boys” leo inatarajia kucheza dhidi ya timu ya vijana ya Madagascar kwenye mechi ya kirafiki itakayofanyika katika uwanja wa taifa wa Madagascar.

Serengeti Boys ipo ziarani jijini Antananarivo nchini Madagascar kujiandaa kucheza na Afrika Kusini katika mchezo wa awali wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Serengeti Boys: Wakishangilia moja ya magoli yao.Serengeti Boys: Wakishangilia moja ya magoli yao.

Mchezo wa marudiano dhidi ya Afrika Kusini utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara nchini India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *