Serengeti Boys leo inatarajia kushuka dimabni dhidi ya Mali kwenye mechi ya kwanza ya michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Serengeti Boys imepangwa katika Kundi B, ambapo katika kundi hilo iko pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zinacheza leo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa kikosi cha Serengeti Boys kiko vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa mali kwenye mchezo huo wa kwanza.

Timu hiyo ya Taifa ya vijana pamoja na maandalizi mazuri lakini imepata pigo baada ya nahodha, Abd Makamba kuvunjika mguu hivyo hataweza kushiriki mashindano yote.

Mechi hiyo itakuwa kali kutokana ubora wa timu ya Mali ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa kombe hilo la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Mechi hiyo inatarajia kuanza mida ya saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika miji wa Libreville nchini Gabon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *