Serena williams ametolewa nje ya mashindano ya michezo ya Olimpiki baada ya kufungwa na Elina Sitoniva kutoka Ukrane katika hatua ya tatu ya tenisi ya mashindano ya wanawake.

Serana amefungwa kwa seti 6-4-6-3 na Sitoniva ambae anashika nafasi ya 20 kwa ubora duniani.

Bingwa huyo wa dunia alionekana kufanya makosa mara tano mfululizo katika raundi ya saba kipindi cha pili.

 Baada ya mchezo huo kumalizika Serena amesema kwamba Sitoniva ni mchezaji mzuri na ndiyo mana ameshinda lakini anajua kuwa wakati mwingine utakua mchezo mzuri sana na anadhani atamshinda.

Serena na ndugu yake Venus wametolewa katika mashindano ya wawili ya wanawake siku ya jumapili na raia wa jamhuri ya watu wa Cze, Lucie Safarova na Barbora Strycova.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *