Mchezaji nyota wa tenisi nchini Marekani, Serena Williams ameweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mmoja wa waanzilishi wake Alex Ohanian kwenye mtandao wa kijamii.

Kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii Serena ameeleza jinsi Alex alivyompeleka katika mgahawa mmoja mjini Rome nchini Italia eneo ambalo walikutana kwa mara ya kwanza mwaka jana.

williams

Serena amesema kuwa siku hiyo alivalishwa pete kwenye kidole chake na kusema maneno manne na yeye akasema ndio kwa mpenzi wake huyo.

Ikumbukwe mwezi julai mwaka huu Serena alishinda medali ya Wimbledon kwa mara ya saba na mwezi wa tisa aliweza kuchukua nafasi ya Roger Federer ambaye alikuwa mshindi wa mechi za Grand MATCH kwa kipindi kirefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *