Seneta wa Australia, Larissa Waters amekuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo.

Bi Waters kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha Green Party alimnyonyesha mwanawe wa miezi miwili Alia Joy wakati wa kura siku ya Jumanne.

Bunge mwaka uliopita lilijiunga na seneti kuruhusu kunyonyesha, lakini hakuna mbunge ambaye alikuwa amewahi kufanya hivyo.

Hatua hiyo inajiri baada ya Kelly O’Dwyer, waziri wa serikali 2015 kutakiwa kutoa maziwa ili kutokosa vikao vya bunge.

Hadi kufikia mwaka uliopita, wabunge katika bunge dogo walikuwa wanaweza kuwabeba watoto wao na kuingia katika afisi za bunge pekee ama maeneo ya uma.

Mnamo mwaka 2016, mbunge wa Uhispania Carolina Bescansa kutoka chama cha Podemos alikosolewa na kupongezwa wakati huohuo kwa kumpeleka mwanawe bungeni na kumnyonyesha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *