Senegal yaibamiza Zimbabwe 2-0 na kutinga robo fainali Afcon

0
209

Senegal imekuwa timu ya kwanza kufuzu robo fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Zimbabwe kwenye mechi iliyofanyika jana.

Goli la kwanza kwenye mechi hiyo limefungwa na mshambuliaji wa Liverpool Saido Mane dakika ya tisa baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na mshambuliaji wa Lazio Keita Balde Diao.

Goli la pili limefungwa na Henri Saivet anayechezea klabu ya St Etienne kwa mkopo akitokea Newcastle baada ya kupiga faulo moja kwa moja na kutinga wavuni ikiwa ni umbali wa mita 20 kwenye dakika ya 13.

Kutokana na matokeo hayo Senegal inaongoza kundi B ikiwa na alama 6 baada ya kucheza mechi mbili na kushinda zote.

Nafasi ya pili kwenye kundi hilo inashikiliwa na Tunisia mwenye alama 3 baada ya kushinda mechi moja na kupoteza moja huku Algeria na Zimbabwe zikiwa na alama 1 kila mmoja.

LEAVE A REPLY