Staa wa pop nchini Marekani, Justin Timberlake nusura akabiliwe na mashtaka baada ya kupiga picha (Selfie) kwenye eneo la kupigia kura lililopigwa marufuku.

Timberlake amejipiga picha hiyo wakati akipiga kura katika mji wa Memphis, Tennessee nchini Marekani.

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa mamilioni ya wapiga kura ambao wamekuwa wakipiga kura zao mapema nchini humo.

Timberlake hakuwa anakumbuka kwamba jimbo la Tennessee lilipiga marufuku upigaji wa picha katika vituo vya kupigia kura mwaka jana.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa eneo la Shelby awali imesema imefahamishwa kuhusu uwezekano wa uvunjaji wa sheria za uchaguzi na kwamba kisa hicho kilikuwa kinachunguzwa.

Lakini baadaye, mwanasheria wa jimbo hilo, Amy Weirich amesema taarifa hiyo ya awali haikuwa sahihi na lilitolewa kwa umma bila yeye kufahamu.

Mwanamuziki huyo kama angefunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria za uchaguzi, angehukumiwa kufungwa jela siku 30 au kupigwa faini $50 (£41), au apewe adhabu zote mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *