Mwanamuziki nyota wa pop nchini Marekani, Selena Gomez ni msanii aliyepata umaarufu zaidi katika mtandao wa Instagram mwaka huu.

Selena anawafuasi wengi zaidi na pia ana picha nane kati ya 10 zilizopendwa zaidi na watumiaji wa mtandao huo mwaka huu.

Instagram kwenye takwimu zake za mwaka huu zinasema wasanii wa kike ndio waliofanikiwa zaidi katika mtandao huo kulinganisha na wanaume.

Selena Gomez ana wafuasi 103 milioni na kuwazidi mastaa wengine wanaotumia mtandao huo wa Instagram.

Mbali na Selena Gomez wengine wenye wafuasi wengi ni nyota mwenzake wa Pop Taylor Swift ambaye ana wafuasi 94 milioni.

Wengine ni Ariana Grande na Beyonce kisha mwigizaji wa kipindi cha uhalisia cha  runinga na mwanamitindo mashuhuri nchini Marekani, Kim Kardashian.

Nafasi ya sita inashikiliwa na mchezaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo akishika namba kwa upande wa wanaume.

Picha ya Selena Gomez iliyopendwa zaidi na kumpa umaarufu katika mtandao huo ni moja ambapo anakifanya tangazo la Coca-Cola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *