Wimbo wa Alikiba ‘Seduce Me’ umerudi nafasi ya kwanza katika mtandao wa Youtube baada ya kushushwa jana na wimbo wa ‘Zilipendwa’ kutoka WCB.

Zilipendwa kutoka kwa ‘WCB’ jana ulipanda kwenye nafasi hiyo ya kwanza lakini haukudumu sana ambapo leo umeshushwa mpaka nafasi ya pili.

Nyimbo hizo zilitoka siku moja Ijumaa iliyopita ila zilipishana masaa tu ambapo Alikiba ndiyo alianza kuachia wimbo wake huo wa ‘Seduce Me’ na baadae Diamond Platnumz akiwa na WCB waliachia ‘Zilipendwa.

Mpaka sasa wimbo wa Alikiba umefikisha views milioni tatu ndani ya siku tano huku wimbo wa Zilipendwa ukiwa na views zaidi ya milioni mbili.

Alikiba kupitia wimbo wake huo alikaa katika nafasi hiyo ya uongozi kwa siku tano kabla ya kushushwa hapo jana na wimbo wa ‘Zilipendwa’ wa WCB.

Mpaka sasa ‘Seduce Me’ tayari umejitengenezea rekodi kadhaa kwenye mtandao huo ikiwemo kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 38.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *