Mahakama ya wilaya ya Ilala leo imeshindwa kusikiliza kesi ya unyang’anyi na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete  (33) maarufu kama Scorpion.

Kesi hiyo imehairishwa baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo Flora Haule kuwa na udhuru na kushundwa kuhuduria mahakamani.

Kesi hiyo inayoendeshwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ilipaswa kuendelea leo Agosti 24 kwa upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga ameiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya upande wa utetezi kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi, lakini Hakimu anayesikiliza shauri hilo amepata udhuru hivyo, hivyo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Adelf Sachore ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea.

Ikumbukwe Agosti 2 mwaka huu Shahidi wa tisa katika kesi ya hiyo, aliieleleza Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alikiri kosa la kumjeruhi Saidi Mrisho, wakati akihojiwa kwenye kituo cha Polisi Buguruni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *