Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemfutia shtaka linalomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ baada ya upande wa mshtaka kuomba shitaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Aderf  Sachore amekubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa mamlaka mkurugenzi wa  mashtaka nchini (DPP) kuondoa shitaka mahakamani muda wowote ilimradi kesi hiyo kama ijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa mamlaka DPP kumshtaki mshitakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendelea na shitaka hilo.

Njwete maarufu kama Scorpion anakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho.

Lakini shitaka hili limefutwa hata hivyo anaweza kufunguliwa shitaka lingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *