Kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger ameachwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya mashindano ya Europa Ligi msimu huu.

Jana kiungo huyo alijumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United kwa jili ya kushiriki ligi kuu nchini Uingereza lakini leo jina lake limekosekana kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya Ulaya.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aliamua kumpeleka kiungo huyo kwenye kikosi cha pili cha Mashetani hao kwa ajili ya kupandisha kiwango chake ambacho kimetetereka kwasasa.

Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kutumia timu ya taifa ya Ujerumani miaka 12 ambapo amecheza mechi 121 na kushinda magoli 24.

Schweinsteiger alisaini mkataba wa miaka mitatu mwaka jana na Manchester United chini ya kocha Louis Van Gal akitokea mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *