Nahodha wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger amecheza mechi yake ya mwisho kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Finland baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa.

Kiungo huyo wa Manchester United alianza kuichezea Ujerumani kuanzia mwaka 2004 ambapo amecheza mechi 121 na kushinda magoli 24.

Mchezaji huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Argentina kwenye mechi ya fainali.

b3

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney amempongeza mchezaji huyo kwa kustaafu soka la kimataifa pamoja na mchezaji wa zamani wa Ujerumani Didi Hamann pia alimponza Schweinsteiger.

 Kwa upande mwingine Schweinsteiger amekanusha kwamba ana mgogoro na kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ambapo amesema anataka kucheza kwenye kikosi cha Unired licha ya kukosa namba kikosi cha kwanza.

B1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *