Kipa wa klabu ya Leicester Kasper Schmeichel amesema kuwa timu hiyo huenda ikashuka daraja iwapo itaendelea kupoteza mechi zake.

Klabu hiyo wapo nyuma kwa pointi moja juu ya timu zilizopo katika orodha ya timu zitakazoshushwa daraja baada ya kufungwa 3-0 na Manchester United.

Leicester haijashinda mechi hata moja mwaka huu 2017 na hawajafunga hata bao moja katika mechi tano ilizocheza.

Wakati kama huu mwaka uliopita, Leicester ilishinda 3-1 katika uwanja wa Etihad dhidi ya Manchester City na kupanda juu ya msimamo wakiwa na pointi tano kabla ya kushinda taji la ligi.

Klabu hiyo ina pointi 38 nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea huku ripoti zikisema kuwa kocha wao  Claudio Ranieri hapendwi tena na wachezaji wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *