Serikali ya Saudia Arabia imeruhusu wanawake nchini humo kuendesha magari kwa mara kwa historia ya nchi hiyo.

Ruhusa hiyo imetolewa na Mfalme Salman bin Abdulaziz na itabaki kuwa historia kwa taifa hilo.

Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.

Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari kwa muda mrefu.

Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi June mwakani na kwa sasa Wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *