Muigizaji mkongwe wa bongo movie, Sandra amesema kuwa wasanii wapya walioingia kwenye uigizaji ndiyo chanzo cha tasnia hiyo kushuka kwasasa kutokana na kukosa maadili.

 

Muigizaji huyo amesema kuwa wasanii wengi wanaingia katika tasinia ya bongo movie kwa malengo ya kupata umaarufu ili wapate njia za kufanya mambo yasiyofaa katika jamii kupitia umaarufu walioupata.

 

Sandra amesema watu wanaopata skendo mbaya kupitia umaarufu walioupata ndani ya bongo movie wanasababisha kupoteza heshima za wasanii wanaojiheshimu lakini pia inaharibu tasnia nzima ya bongo movie na kunyima ajira wasanii wengine.

 

Vile vile Sandra amewasihi na kuwashauri waandaaji wa bongo movie kuangalia watu wa kuwaweka katika movie lakini pia amewasihi wasanii wanaoingia katika tasinia wachague sehemu ambazo zinamfaa kuigiza ili kuweza kurudisha soko la bongo movie na kuwafurahisha mashabiki.

 

Muigizaji huyo alipata umaarufu kutokana na uigizaji wake katika soko zima la filamu filamu zilizompa umaarufu ni ‘Misukosuko’ sehemu ya kwanza na ya pili vile vile ni mmoja wa waigizaji wa kundi la Kaole Sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *