Muigizaji mkongwe wa Marekani, Samuel L. Jackson amesema kuwa watu wamekuwa na shauku kumuona anaondoka Marekani baada ya Trump kushinda kiti cha urais nchini humo.

Kauli hiyo inakuja baada muigizaji huyo kusema kuwa kama Donald Trump atashinda urais nchini Mareakani basi atahamia AFrika Kusini na sasa.

 Baaddi ya watu wa Afrika Kusini kupitia mtandao wa Twitter wanataka kujua lini staa huyo ataondoka Marekani na kurejea Afrika Kusini.

Mtandao wa twitta nchini Afrika Kusini ulipamba moto kwa jina la muigizaji Samuel L. Jackson wakitaka kujua anakuja lini nyumbani kwao baada ya Trump kushinda.

Kupitia akaunti yake ameandika “Kwanini kunashauku kubwa ya mimi kuondoka, nalipa kodi nyingi zaidi kuliko nyie wa tu wa Trump na hata huyo Donald Trump mwenyewe”.

Mbali naMuigizaji huyo kusema atahama Marekani kama Trump atashinda urais nchini humo wengine waliosema kauli hiyo mwanamuziki, Neyo pamoja na muandishi wa vitabu Profesa Wole Soyinka ambaye atahama baada ya Trump kuapishwa mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *