Kampuni ya Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.

Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.

Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.

Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky, Marekani anasema aliamka na kupata chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.

Siku chache awali, abiria kwenye ndege moja Marekani walitakiwa kuondoka kwa dharura ndegeni baada ya simu ya Note 7 kuanza kutoa moshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *