Samia: Tujifunze China kukuza uchumi

0
161

Serikali imesema iko tayari kujifunza namna ambavyo China imefanikiwa katika kukuza uchumi wake, ili kutengeza mfumo utakaoleta maisha bora kwa Watanzania wote.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua sherehe za Mwaka Mpya wa China, ambao kwa mwaka huu unajulikjana kama ‘Mwaka wa Jogoo” katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Samia amesema mafanikio ya China katika kuwatoa wananchi wake katika umasikini, unaendelea kuihamasisha Serikali na hasa katika kipindi hiki ambacho inaongia katika mageuzi ya kiuchumi.

Amesema uhusiano kati ya China na Tanzania ni wa muda mrefu na kwamba wanathamini mchango mkubwa wa China katika maendeleo ya Tanzania.

Akizungumzia nyanja ya kisiasa, alisema ubadilishanaji uzoefu baina ya nchi hizo mbili hasa katika masuala ya utawala, umeongezeka na kuzaa matunda.

Alisema ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ilikuwa si tu kwajili ya kuboresha mahusiano ya kidiplomasia pekee, bali pia kufanya kazi ya kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na mikakati ya miradi ya miundombinu, ambayo ni muhimu katika kusaidia maendeleo ya viwanda nchini.

LEAVE A REPLY