Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva imeikumbusha serikali mambo matatu.

Makamo wa Rais amesema hayo jana wakati wa kuaga miili ya marehemu hao katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha ambapo aliongoza waombolezaji kuaga miili hiyo.

Jambo la kwanza alilosema makamo wa Rais ni kupiga marufuku utumiaji wa vilevi na madawa ya kulevya kwa madereva pindi wanapokuwa barabarani kutokana na vitu hivyo kuchangia kutokea kwa ajali nyingi nyingi.

Jambo la pili amesema serikali itajitahidi kuweka vizuri alama za barabarani ili madereva wazingatie alama hizo na kuepuka ajali zisizo na sababu.

Jambo la tatu amesema kuwa kuwa madereva wahakikishe wanapakia abiria ambao wanastahili kwa gari husika na si kuzidisha abiria kwa tamaa za fedha.

Ajali hiyo imetokea May 6 mwaka huu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *