Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiomba Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kuanzisha kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa tezi dume kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofariki sasa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jana mkoani Mwanza wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya shingo ya kizazi na saratani matiti.

 

Amesema kuwa kati ya watu saba, wanne wanafariki dunia kutokana na tezi dume ambayo huwapata wanaume.

 

Akizungumzia saratani ya kizazi na ya matiti Makamu Rais alishauri jamii hasa akina mama kupima afya zao ili kuepuka matatizo hayo ambayo yamekuwa yakiongoza kwa vifo vya watu wengi.

 

Amebainisha kuwa serikali kwa kutambua hilo imetoa shilingi bilion tano ili kujenga vituo vitatu vya afya katika kila halmashauri nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *