Kocha wa timu ya taifa, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 24 watakaoanza maandalizi ya kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba wa michuano ya AFCON dhidi ya Nigeria.

Wachezaji hao walioitwa na Mkwasa wanatakiwa kuripoti kambini Julai 31 mwaka huu na kuanza kambi ya siku tano itakayomalizika August 5 2016.

Hata hivyo kuelekea mchezo huo dhidi ya Nigeria utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi Septemba utawakosa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

 Magolikipa

Deogratus Munish, Beno Kakolanya (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) Mabeki Oscar Joshua,  Kelvin Yondani, Juma Abdul (Yanga), Erasto Nyoni, Agrey Morris (Azam FC) Mohamed Hussein (Simba ).

 Viungo
Farid Musa, Himid Mao (Azam FC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude (Simba), Ibrahim Rajab ‘Jeba’ (Mtibwa Sugar ), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Simon Msuva, Juma Mahadh (Yanga ).

 Washambuliaji
Joseph Mahundi (Mbeya City), Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate (Simba), John Bocco (Azam FC) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Taifa Stars: Kikosi cha timu ya taifa
Taifa Stars: Kikosi cha timu ya taifa

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *