Timu ya taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) leo imeshinda 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mgoli yote ya Taifa Stars yamefungwa na mshambuliaji wa klabu ya Genk Mbwana Samata katika dakika ya 3 na 87 ya mchezo huyo.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizikia Stars walikuwa mbele kwa goli moja kwenye mechi hiyo ya aina yake.

Taifa Stars wameonekana kumiliki sana mpira kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho kwenye mchezo huo licha ya kukosa magoli mengi.

Mbali ya mchezo huo hii leo Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo Machi 28  mwaka huu, mchezo ambao pia ni wa kirafiki wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *