Mbwana Samatta anaendelea kung’ara nchini Ubelgiji baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, yeye akifunga goli mbili dhidi ya Lokeren.

Samatta aliifungia timu yake magoli katika dakika ya 34 na 38,huu ulikuwa mchezo wa nne kwa klabu yake Ligi kuu ya Ubelgiji wakiwa wanashinda michezo miwili huku mchezo yote walioshinda Samatta amefunga goli, kufungwa moja na kutoka sare mmoja.

Samatta: Akishangilia goli na mchezaji mwenzake wa Genk.
Samatta: Akishangilia goli na mchezaji mwenzake wa Genk.

Kwa matokeo hayo Genk wanapanda nafasi ya nne na kuwa na pointi 7 huku Samatta akiwa na magoli manne ya Ligi pamoja na matatu ya Europa Ligi kwa sasa ndo anaongoza ufungaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *