Samaki Mkubwa aina ya Nyangumi amekutwa akiwa amekufa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Ripiti kutoka eneo la tukio zinasema Nyangumi huyo alianza kuonekana akielea baharini tangu jana na leo alfajiri alisukumwa hadi ufukwe huo katika bandari ya wavuvi.

Mmoja wa wananchi katika eneo hilo, Akram Kidudu amesema kuwa bado haijajulikana chanzo cha kifo cha nyangumi huyo na polisi wapo eneo la tukio kuzuia wananchi wasianze kugawana kitoweo hicho bila kujua usalama wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *