Mwanamuziki wa Bongo Flava, Sam wa Ukweli amefunguka kwa kusema sababu iliyomfanya akae kimya kwa kipindi cha muda mrefu ni lebo yake ya Al Jazeera.

Mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo yake ‘Sina Raha’ amesema kuwa Al Jazeera ndiyo iliyosababisha awe kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo mpaka kupelekea kupotea kwenye game la muziki.

Sam wa Ukweli amesema kuwa alitaka kuvunja mkataba na lebo hiyo kutokana na kuona hakuna kazi iliyokuwa inafanyika hivyo alitaka kuwa huru lakini ikashindikana.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa kama angevunja mkataba huo alitakiwa alipe shilingi milioni 100 ili atoke kwenye lebo hiyo ndiyo mana akaa kimya muda mrefu.

Mkataba wake na lebo hiyo kwasasa umeshamalizika na yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote kama watakubaliana kwenye mkataba.

Sam wa Ukweli ni mwanamuziki aliyeanza game miaka ya nyuma iliyopita wakati huo akishindanisha na Diamond Platnumz ambaye mwenzake sasa ni msanii mkubwa barani Afrika wakati walianza muziki sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *