Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ameiwezesha klabu yake kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwafunga Manchester City 2-1 kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Salah ameisadia Liverpool kutinga hatua hiyo baada ya miaka 10 kufanya hivyo na sasa wametinga tena.

Katika mchezo uliofanyika jana, Manchester City ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli la mapema kupitia mshambuliaji wake, Gabriel Jesus baada ya kupokea pasi kutoka kwa winga Rahim Sterling.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Manchster City walikuwa mbele kwa goli hilo moja huku Liverpool wakiwa hawana hawana kitu.

Liverpool wakafanikiwa kusawazisha kupitia mshambuliaji wake hatari Mohamed Salah baada ya mabeki wa City kujichanganya.

Goli la Pili la Liverpool lilifungwa na mshambuliaji raia wa Brazil Roberto Frimino na kufanya matokeo kusomeka 2-1 na matokeo ya jumla kwa mechi mbili kusomeka 5-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *