Staa wa Bongo Fleva ambaye hakuwepo wakati watuhumiwa wa uuzaji, utumiaji na usambazaji wa dawa za kulevya walipotangazwa na kisha kufanyiwa mahojiano kwenye kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaa, Vanessa Mdee ‘amefikishwa central’.

Kwa mujibu wa wakili wake, Aman Tenga, Vee Money ameamua kujisalimisha mwenyewe baada ya kupata taarifa ya kuhitajika polisi kwaajili ya mahojiano.

Kwa mujibu wa orodha iliyosomwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Vanessa Mdee naye anatuhumiwa kuhusika kwa namna fulani kwenye sakata hilo.

Tayari kikosi cha maafisa usalama kinadaiwa kukagua makazi ya staa huyo wa Bongo Fleva na kisha kumpeleka staa huyo kwa mkemia mkuu kwaajili ya uchunguzi.

Wakati wa kutajwa kwa orodha ya mastaa wanaotuhumiwa kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya, Vanessa Mdee alikuwa nchini Afrika Kusini akiendelea na shughuli za kikazi.

Bado haijawekwa wazi endapo staa huyo atalazimika kulala kituoni hapo kama walivyolala baadhi ya mastaa wengine au ataruhusiwa kuondoka baadha ya mahojiano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *