Baada ya kuandika barua ya kujiuzulu ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro, aliyekuwa  Mkuu wa Mkoa huo, Said Mecki Sadiki afunguka sababu ya kuachia ngazi nafasi hiyo.

Sadiki amesema kuwa ameamua kuondoka serikalini baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki.

Aidha Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dk John Pombe Magufuli kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa.

Sadiki alisema hayo jana wakati akitaja sababu zilizochangia kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

Amesema Sababu nyingine kubwa ni kuhofia afya yake kutomudu kasi ya rais Magufuli kwani alifanywa upasuaji mwaka 2012 na 2014 nchini India.

Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi kujitathmini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *