Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili, Saida Karoli amewamwagia sifa kedekede wasanii wa Bongo Fleva, Ray C na Darassa kutokana na nyimbo zao kubamba sana masiki mwa watu.

Saida amesema kuwa wimbo wa Darassa ‘Muziki’ ni vigumu kuja kushuka na kuwataka wasanii wengine hasa wa hip hop kuchukulia hilo kama somo.

Mwanamuziki huyo pia amesema kuwa Ray C licha ya msanii huyo kupitia matatizo mengi bado uwezo wake upo pale pale na kuna baadhi wamejaribu kumuiga ila wameshindwa.

Saida amesema kuwa “Kwa kweli Ray C nampenda sana kutoka moyoni tangu zamani, sauti yake ni nzuri haina mpinzania, wasichana wengi wamejaribu kuiga kuimba kama yeye, wanapenda mvuto wake na muonekano wake lakini wameshindwa.

Pia ameongeza kusema kuwa  “Na ukiangalia Ray C amepitia matatizo makubwa sana hapa katikati lakini napenda kumshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipomsaidia Ray C.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *