Kijana Said Mrisho aliyetobolewa macho na Scorpion leo amefika mahakma ya Wilaya ya Ilala kutoa ushahidi wa kesi yake dhidi ya Scorpion akiwa kama shahidi namba moja.

Said Mrisho ametoa ushahidi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala na kuiambia mahakama kisa chote kilichotokea hadi kutobolewa macho hayo.

Baada ya kusikiliza hoja za shahidi huyo, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule ameahidi kuwa ataendelea kusikiliza mashahidi wengine wa kesi hiyo.

Kwa upande wa mshitakiwa, Salum Njwete ‘Scorpion’ hakutakiwa kujibu chochote zaidi ya kusikiliza na kurudishwa lupango.

Kesi hiyo imeahirisha ambapo itasikilizwa tena Desemba 27 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *